บทที่ 2 · Jifunze Kichina: Hatua ya Kwanza
Namba 1 hadi 10
Amani Odhiambo · 1 ต.ค. 2569 · 3.1K ครั้งที่อ่าน
Leo tutahesabu kwa Kichina. Namba za Kichina ni rahisi kukumbuka.
一 (yī) moja, 二 (èr) mbili, 三 (sān) tatu, 四 (sì) nne, 五 (wǔ) tano.
六 (liù) sita, 七 (qī) saba, 八 (bā) nane, 九 (jiǔ) tisa, 十 (shí) kumi.
Angalia: namba moja, mbili na tatu zina mistari kama idadi yake. Moja ni mstari mmoja, mbili ni mistari miwili.
Zoezi: Hesabu vidole vyako kwa Kichina kutoka 一 hadi 十.
ยังไม่มีความคิดเห็น เป็นคนแรกที่พูดคุยเกี่ยวกับเรื่องนี้